Utafiti: Trump na Sera zake hana umaarufu duniani

Ulimwengu wa rais Donald Trump wa Marekani
Image caption Ulimwengu wa rais Donald Trump wa Marekani

Utawala wa rais Donald Trump umekuwa na athari kubwa kuhusu vile ulimwengu unavyoiona Marekani kulingana na utafiti uliofanywa.

Utafiti huo uliofanywa na shirika la Pew Research Center uliwahoji zaidi ya watu 40,000 katika mataifa 37 mwaka huu.

Ulibaini kwamba rais wa Marekani na sera zake hana umaarufu duniani.

Utafiti huo unaonyesha ni mataifa 2 kati ya 37 ambayo yanampendelea rais Obama ikilinganishwa na mtangulizi wake Barrack Obama: Israel na Urusi.

Lakini ripoti hyo inaonyesha kwamba watu wengi wanahisi kwamba uhusiano wao na Marekani hautabadilika katika kipindi cha miaka ijayo.

Vitu muhimu vilivyobainika katika utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe 16 Februari na 8 Mwezi Mei vinashirikisha: Raia kuwa na imani chache na Trump ikilinganishwa na Obama.

Watu walihojiwa mwishoni mwa utawala wa rais Obama , na baada ya kuanza kwa utawala wa Trump waliulizwa iwapo walihisi wana imani kwamba rais Trump atafanyia ulimwengu mambo wanayoyataka ya ulimwengu.