Malkia Elizabeth apata nyongeza ya mshahara ya £6m

Malkia Elizabeth apata nyongeza ya mshahara Haki miliki ya picha EPA
Image caption Malkia Elizabeth apata nyongeza ya mshahara

Malkia wa Uingereza anatarajiwa kupokea asilimia 8 ya nyongeza ya mshahara kutoka kwa fedha za umma baada ya biashara ya ufalme huo kupata faida iliopanda kwa pauni milioni 24.

Ufadhili huo ambao humlipia mishahara ya ufalme wake, uchukuzi na marupurupu unatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya pauni milioni 6 mwaka 2018/19.

Inajiri huku akaunti zikionyesha kuwa matumizi ya malkia mwaka uliopita yalipanda kutoka pauni milioni mbili hadi pauni miolini 42.

Alan Reid ambaye ni msimamizi wa fedha hizo alisema kuwa Malkia aliwakilisha utumizi mzuri wa fedha.

Ufadhili huo unatolewa kila bada ya miaka miwili ,ni fedha anazopewa malkia na wizara ya fedha.

Zinatokana na faida za biashara za malkia ambazo zinashirikisha eneo kubwa la West End mjini London.

Biashara hizo zilimpatia malkia faida ya pauni milioni 24.7 hadi pauni milioni 328.8 mwaka 2016/17