Al-Shabab wamtafuta aliyekuwa kamanda wao

Abu Mansur alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabab na pia alihudumua kama msemaji wa kundi hilo. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Abu Mansur alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabab na pia alihudumua kama msemaji wa kundi hilo.

Wapiganaji wa al-Shabab wanaripiwa kumtafuta aliyekuwa mmoja wa makamanda wake, Sheikh Muqtar Ali Abu Mansur, ambaye aliondolewa zawadi iliyotangazwa na Marekani ya dola milioni tano siku kadhaa zilizopita.

Kundi la al-Shabab linaamini kuwa Abu Mansur ana mipango ya kujisalimisha kwa serikali ya Somalia ambayo wanaipinga, kwa hivyo sasa wanamtafuta.

Anaaminika kujificha kusini magharibi mwa Somalia.

Abu Mansur alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabab na pia alihudumua kama msemaji wa kundi hilo.

Alipata mafunzo ya jihadi kwenye kambi nchini Afghanistan, kwa mujibu wa maafisa nchini Somalia.

Hata hivyo tofauti ziliibuka kati yake na viongozo wengine wa al-Shabab, na tangu wakati amekuwa kwenye mazungumzo na serikali.