Google yapigwa faini ya dola bilioni 2.7 kwa kukiuka sheria za mauzo

Google Shopping Haki miliki ya picha Google
Image caption Matangazo ya Google huoneka kwanza mtu anapotafuta

Google imepigwa faini ya ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kuamua kuwa Google ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.

Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.

Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi.

Haki miliki ya picha European Commission
Image caption Margrethe Vestager alisema kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU

Kampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa.

Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo.

"Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU," alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Matangazo huyasukuma mengine nje hasa kwenye simu

Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya bioshara ya Google tangu mwaka 2010

Uchunguzi huo ulianza kufuatia malalamiko kutoka makampuni kama Microsoft miongoni mwa mengine.

Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Google

Mada zinazohusiana