Jinsi magari yasiyo na dereva hukanganywa na kangaroo.

Kangaroo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jinsi magari yasiyo na dereva huchanganywa na kangaroo.

Magari ya Volvo yanayojiendesha yenyewe yamekuwa na wakati mgumu kutambua Kangaroo wakiwa barabarani.

Magari ya kampuni hiyo ya Sweden ya mwaka 2017 ya S90 na XC90 hutumia teknolojia yake ya kutambua wanyama barabarani.

Lakini jinsi ambavyo kangaroo hutembea huyachanganya magari hayo.

"Tumegundua kuwa kangaroo akiruka huonekana ni kana kwamba yuko mbali, na wakati anapotua ardhini huekana akiwa karibu," meneja wa kiufundi nchini Australia aliliambia shirika la ABC.

Haki miliki ya picha Volvo
Image caption Volvo imekuwa ikifanyia majaribio mifumo ya kutambua kangaroo tangu mwaka 2015

Kulingana na halmashauri ya barabara nchini Australia, ni kuwa asilimia 80 ya ajali za magari na wanyama nchini humo uhusisha kangaroo

Zaidi ya ajali 16,000 za kangaroo kila mwaka, huchangia madai ya mamilioni ya dola kama bima.

Wahandisi walianza kurekodi mienendo ya kangaroo katika eneo litalotambulia kuwa lenye ajali nyingi mwaka 2015.

Takwimu hizo zitatumiwa kuunda teknolojia na kamera ambazo zitaweza gari kutambua kangaroo na kushina breki ikiwa kuna hatari ya kutokea ajali.