WFP yahitaji fedha zaidi kukabiliana na njaa haswa kwa watoto

WFP inasema kuna upungufu mkubwa wa chakula sehemu zenye vita
Image caption WFP inasema kuna upungufu mkubwa wa chakula sehemu zenye vita

Mkuu mpya wa shirika la chakula duniani (WFP) David Beasley ametaka kuongezwa fedha zaidi zitakazonunua vyakula vya kutosha ili kusaidia mamia ya watoto wanaokufa kwa njaa duniani.

Amesema nchi nne zilizoathirika zaidi ni Yemen, Sudan Kusini, Somalia na Nigeria, na kuna uwezekano watoto mia sita wakafariki ndani ya miezi minne ijayo kwa kukosa chakula.

Ameitaka pia Saudi Arabia kuisaidia Yemen kukabiliana na baa kubwa la njaa linaloikabili.

Vita inatajwa kuwa sababu kubwa ya watoto kukosa chakula katika sehemu zenye migogoro.