Maseneta Marekani wazuilia mswada wa bima ya Obama

Chini ya mfuko huo, mamia ya watu wanapata huduma ya matibabu bure
Image caption Chini ya mfuko huo, mamia ya watu wanapata huduma ya matibabu bure

Maseneta wa Republican nchini Marekani wamesitisha kura dhidi ya mswada uliyopendekezwa wa bima ya matibabu.

Tangazo kutoka kwa kiongozi wa wengi katika bunge hilo, Mitch McConnell, amesema ni pigo jingine kwa juhudi za Republican kufanyia marekebisho bima ya matibabu iliyobuniwa na Barak Obama.

Seneta McConnell alikuwa na mpango wa mswada huo kupigiwa kura wiki hii, lakini maseneta watano wa Republican wamesema wataupinga mswada huo na wakati ambapo chama hicho kinahitaji kura mbili zaidi kupitatisha mswada huo katika bunge la juu.

Image caption Baadhi ya watu wamekuwa wakipinga kuondolewa kwa huduma hiyo.

Rais Donald Trump amekutana na maseneta wa Republican katika ikulu ya White House hatua ambayo Bw McConnell amesema itasidia pakubwa katika mchakato wa kuwapatia wamarekani bima mbadala ya matibabu itakayochukua nafasi ya ile iliyopo sasa.