Serena Williams apiga picha za utupu akiwa mjamzito

Mchezaji wa tenisi Serena Williams
Image caption Mchezaji wa tenisi Serena Williams

Mchezaji wa tenisi anayeorodheshwa nambari miongoni mwa wanawake Serena Williams amepiga picha za utupu katika kurasa ya kwanza ya jarida la August Vanity Fair.

Nyota huyo wa tenisi alibaini kwamba alikuwa akitarajia mwanawe wa kwanza na mpenziwe Alexis Ohanian kabla ya michezo ya Australia Open mnamo mwezi Januari.

Aliambia jarida hilo kwamba hakutarajia chochote hadi alipobaini kwamba alikuwa mgonjwa wakati wa mazoezi.

Haki miliki ya picha Vanity fair
Image caption Picha ya utupu ya Serena katika jarida la vanity fair

Lakini rafikiye alishuku kwamba huenda ni mjamzito na kuamua kuchukua vipimo.

Serena alifanya vipimo hivyo wakati alipokuwa akipigwa picha na kampuni moja ndani ya Hoteli moja nchini Australia na kusema kuwa alipigwa na butwaa wakati alipopata majibu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serena Wiliams na mpenzi wake Alexis Ohanian

''Mungu wangu, hii haiwezekani- ni lazima nicheze mchuano mmoja'',alisema. Nitacheza vipi mashindano ya Australian. Nilikuwa nimepanga kushinda taji la Wimbledon mwaka huu''.

Rafikiye Jessica baadaye alitumwa kununua vifaa vyengine vitano vya kupima uja uzito ili kumthibitishia Serena kwamba ni mjamzito.

Vipimo vyote vilithibitisha.Habari hiyo pia ilisema vile Serena na mpenziwe walivyokutana 2015.

Image caption Serena Williams

Alimchumbia Disemba katika meza hiyo hiyo ya Cavalieri katika hoteli moja huko Italy ambapo walikutana.