Burudani yasababisha polisi 220 kutimuliwa Ujerumani

The entrance of a former barracks ground in Bad Segeberg, near Hamburg, is pictured on June 27, 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Berlin inatuma polisi 1000 kama sehemu ya polisi 20,000 wanaoletwa kulinda mkutano huo ambao utaandaliwa tarehe 7 na 8 mwezi Julai.

Polisi hao walipelekwa kulinda mkutano mjini Hamburg wa nchi tajiri zaidi duniani wiki ijayo lakini sasa wamefukuzwa kwa kuleta aibu.

Polisi hao 220 kutoka mjini Berlin walionekana kwenye kambi yao wakshiriki katika vitendo kama vile ngono na kuenda haja ndoto kwenye ukuta wakiwa wengi.

Wasimamizi wao huko Berlin waliaibishwa na kitendo hicho na kusema kuwa polisi zaidi watatumwa kuchukua mahala pao.

Mkutano wa G20 unatarajiwa kuvutia maandamano makubwa.

Berlin inatuma polisi 1000 kama sehemu ya polisi 20,000 wanaoletwa kulinda mkutano huo ambao utaandaliwa tarehe 7 na 8 mwezi Julai.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi hao 220 kutoka mjini Berlin walionekana kwenye kambi yao wakshiriki katika vitendo kama vile ngono na kuenda haja ndoto kwa ukuta wakiwa wengi.

Burudani zilianza mara tu maafisa 500 walipowasili kutoka Berlin siku ya Jumapili .

Usalama kwenye mkutano wa G20 ulitiliwa maanani zaidi mapema wiki hii wakati Ujerumani ilisema kuwa haitarajii walinzi wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kufika Hamburg.

Mwezi uliopita waandamanaji kadha waliumi kwenye shambulizi nje ya ubalozi wa Uturuki mjini Washington DC.

Walimzi wa Rais Erdogan walikuwa miongoni mwa walinzi 12 wa uturuki waliofunguliwa mashtaka.

Mada zinazohusiana