Mwanasiasa aliyemtishia maisha Rais Bongo akamatwa Gabon

Rais Ali Bongo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Ali Bongo

Mamlaka nchini Gabon imemkamata na kumzuilia mwanasisa wa upinzani baada ya kumtishia maisha Rais Ali Bongo.

Roland Desire Aba'a Minko alikamatwa baada ya kutishia usalama wa taifa, kuchochea mapinduzi na kueneza habari zisizo za ukweli.

Mapema mwezi huu Bwana Aba'a Minko alitisha kulipua mali ya serikali ikiwa bwana Bongo angekataa kuondoka madarakani ndani ya miaka mitatu.

Alisema kuwa Jean Ping ambaye alitangazwa kushinda kwenye uchaguzi wa mwaka uliopita, ndiye kiongozi wa nchi hiyo.

Bwana Aba'a Minko alisimama kama mgombea huru kabla ya kujiondoa na kumuunga mkono Bwana Ping.

Mada zinazohusiana