Israel yashambulia ngome ya Syria siku ya tatu mfululizo

Ni siku ya tatu mfululizo kwa mashambulizi haya
Image caption Ni siku ya tatu mfululizo kwa mashambulizi haya

Israel imeshambulia ngome ya majeshi ya Syria kwa siku ya tatu mfululizo baada ya kombora la wanajeshi hao kuanguka kwa bahati mbaya katika eneo Golan linashikiliwa na Israel.

Katika kisa hicho cha siku ya Jumatano, vikosi vya Israel vilfanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya eneo lao.

Israel imetekeleza mashambulizi kadhaa ya angani mara kwa mara au kujibu mashambulizi wakati wa mzozo wa Syria lakini imejitenga kuhusika moja kwa moja na mzozo huo.

Israel iliuteka mji wa Golan kutoka mikononi mwa Syria wakati wa mapigani ya mwaka 1967.