Helikopta iliyotumika kushambulia mahakama yapatikana Venezuela

Jengo la mahakama lililoshambuliwa
Image caption Jengo la mahakama lililoshambuliwa

Vikosi vya usalama nchini Venezuela vimepata helikopta iliyotumiwa na afisa muasi wa polisi kupaa juu ya majumba ya serikali mjini Caracas huku ikikiangusha guruneti na kupiga risasi siku ya Jumanne.

Image caption Ilikutwa kajika jimbo Vagas pwani kaskazini

Makamu wa rais wa Venezuela, Tareck El Aissami, amesema helikopta hiyo ilipatikana karibu na karibu na jimbo la Vagas pwani kaskazini, kilo mita arubaini na tano kutoka mji mkuu wa Caracas.

Image caption Rais Maduro amekuwa akipata upinzani mkali hivi karibuni na shambulio hilo linatajwa kuwa ni njia ya kumpinga

Aliatoa picha zinzo inayoonyesha helikopta hiyo katika maeneo ya milima ikisafisha maeneo yaliyozungukwa na migomba ya ndizi.

Kufikia sasa hakuna dalili yakupatika na kwa rubani Oscar Lopez, afisa huyo wa polisi huku serikali ikitaja kisa hicho kuwa kitendo cha ugaidi.