Amir wa Dubai asaidia kuwanunulia kanisa wanakijiji

Amir wa Dubai Sheikh MOhammed Al Maktoum asaidia kununua kanisa
Image caption Amir wa Dubai Sheikh MOhammed Al Maktoum asaidia kununua kanisa

Amir wa Dubai Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum amesaidia kijiji kimoja kidogo kulinunua kanisa dogo la Methodist nchini Uingereza.

Wakaazi wa eneo la Godolphin karibu na Helston walimtumia ujumbe kwa lengo la kufanya mchango.

Kijiji hicho kina jina linalofanana na Godolphin Stables kilichoanzishwa na Sheikh huyo kulingana na Cornwal.

Richard Mackie kutoka muungano wa jamii ya Godolphin Cross alisema: Tunamshukuru sana.

Kundi hilo lilihitaji pauni 90,000 kulinunua kanisa hilo ambalo walitaka kulibadilisha na kulifanya kituo cha jamii na walikuwa wamechangisha pauni 25,000.

Haijulikani ni kiwango gani cha fedha kilichotolewa na Sheikh Mohammed ,lakini Mackie alisema ''ametusaidia sana''.

Mwanakijiji mmoja Valerie Wallace alikuwa na wazo hilo kama hatua ya mwisho baada ya kundi hilo kushindwa kuchangisha fedha kutoka maeneo mengine.

''Hatukufikiria wazo kama hilo lakini baadaye tukaanza kupata simu kutoka Abu Dhabi, bwana Mckie alisema. Tulidhani tulikuwa tunafanyiwa mzaha lakini baadaye tukagundua sio kwamwe''.