Waziri mkuu wa zamani wa Israel aliye gerezani Ehud Olmert kuachiliwa

Ehud Olmert (file photo)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Olmert ndiye kiongozi wa kwanza wa zamani nchini Israeli kufungwa jela.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert anaachiliwa mapema kutoka gerezani ambapo anatumikia kifungo cha miezi 27 kutokana na mokosa ya ufisadi

Olmert alifungwa Februari mwaka 2016 na ataachiliwa siku ya Jumapili kwa mujibu wa wakili wake.

Olmert ndiye kiongozi wa kwanza wa zamani nchini Israeli kufungwa jela.

Alichaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 2006 lakini akajiuzulu miaka mitatu baadaye wakati polisi walisema alikuwa na mashtaka ya kujibu.

Olmert mwenye umri wa miaka 71 kwa sasa anachunguzwa kufuatia madai kuwa alitoa sehemu ya kitabu anachoandika nje ya gereza na kuzua hofu kuwa huenda hatua hiyo ikatishia usalama wa taifa.

Wiki iliyopita Olmert alipekekwa hospitalini baada ya kulalamikia maumivu ya kivua.

Mwaka 2014 Olmert alishtakiwa kwa ufisadi kutokana na ujenzi mmoja akiwa meya wa Jerusalem kati ya mwaka 1993 na 2003.