Modi: Msiue kwa jina la "ng'ombe"

Indian PM Narendra Modi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Narendra Modi

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amesema kuwa mauaji kwa jina la ng'ombe ni jambo halitakubalika.

Waumini wengi wa kihindu wanamtambua ng'ombe kuwa myama matakatifu na kuchinjwa kwa ng'ombe kumepigwa marufuku katika majimbo mengi.

Matamshi hayo yanakuja siku chache baada ya kijana mmoja wa kiislamu kuuawa kinyama ndani ya treni na wanaume wa kihindu.

Siku ya Jumatano maelfu ya watu nchini India walishirikia kwenye maandamano kupinga kuongezeka mashambulizi dhidi ya waislamua.

Image caption Siku ya Jumatano maelfu ya watu nchini India walishirikia kwenye maandamano kupinga kuongezeka mashambulizi dhidi ya waislamua.

Wakosoaji wanasema kuwa tangu serikali ya chama cha Hindu nationalist Bharatiya Janata iingie madarakani mwaka 2014, makundi ya kulinda ng'ome yamefanya mashambulizi mengi dhidi ya waislamu nawamuni wa Dalits.

Pia wamemkosoa Bwana Modi kwa kutochukua hatua kukosoa mashambulizi hayo.

Siku ya Alhamisi bwana Modi aliuambia mkutano nyumbani kwake huko Gujarat kuwa kuuawa watu kwa jina la ng'ombe si kuenda na matakaa ya mwanzilishi wa taifa hilo Mahatma Gandhi.