Rais wa TFF akamatwa Tanzania kwa madai ya rushwa

Jamal Malinzi Haki miliki ya picha other
Image caption Jamal Malinzi amekuwa rais wa TFF tangu mwaka 2010

Rais wa shirikisho la kandanda nchini Tanzania (TFF) Jamal Malizia, amekamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo.

Alikamatwa pamoja na katibu wa TFF Selestine Mwesigwa.

Wawili hao walizuiliwa usiku kucha.

Msemaji wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Musa Misalaba aliongeza kuwa wawili hao watabaki kizuizini hadi wahojiwe.

Kukamatwa kwao kunajiri baada ya uchunguzi wa siku nyingi.

Misalaba alisema kuwa idara hiyo inaendelea kuwachunguza maafisa waengine kwa madai sawa na hayo.