Ndege ya rais wa Nigeria yaegeshwa kwa siku 50 London

Rais Muhammadu Buhari (kushoto) na makamu wake Yemi Osinbajo Haki miliki ya picha Nigerian Government
Image caption Rais Muhammadu Buhari (kushoto) na makamu wake Yemi Osinbajo

Ofisi ya Rais nchini Nigeria imekiri kuwa ndege rasmi ya Rais Muhammadu Buhari imeegeshwa kwa zaidi ya siku 50 kwenye uwanja wa ndege mjini London.

Rais Buhari ambaye ni mgonjwa aliondoka nchini Nigeria kwa likizo ya kimatibabu tarehe 7 mwezi Mei akiitumia ndege hiyo.

Ofisi ya Rais ilikuwa ikijibu ripoti za mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu nchini Nigeria, wameelezea ghadhabu yao kutokana na kuegeshea ndegr hiyo mjini London.

Ilidaiwa kuwa ndege hiyo inalipigwa pauni 4000 kwa siku kama ada ya kuiegesha, katika uwanja wa Stansted mjini London, na kwa muda wa siku 50 imegharimu nchi hiyo pauni 200,000.

Msemaji wa rais bwana Garba Shehu, alikana kuwa nchi inalipa pesa nyingi kwa nafasi hiyo. Aliiambia BBC kuwa gharama ya kuegesha ndege hiyo haitazidi pauni 1000.

Rasi Buhari amekuwa nje ya nchi kwa karibu miezi miwili kupata matibabu mjini London.

Mada zinazohusiana