Mkuu wa polisi kuhojiwa kwa matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji Venezuela

Polisi wamekuwa akikumbana na wakati mgumu kukabiliana na waandamanaji
Image caption Polisi wamekuwa akikumbana na wakati mgumu kukabiliana na waandamanaji

Ofisi ya mwanasheria mkuu nchini Venezuela imemtaka mkuu wa zamani wa jeshi la polisi kutoa maelezo juu ya matumizi ya nguzu zilizopitiliza dhidi ya mamiz ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini humo.

Ofisi hiyo imesema kuwa kuna ushahidi wa kutosha juu ya matumizi ya nguvu zilizopitiliza kwa waandamanaji.

Antonio Benavides anatarajiwa kuhojiwa siku Julai sita.

Image caption Antonio Benavides anasema ni vigumu kutumia njia ya kawaida kuwakabili waandamanaji wasiochoka

Aliondolewa madarakani wiki iliyopita, baada ya polisi aliowapa maelekezo kuonekana wakiwafyatulia risasi waandamanaji.

Zaidi ya watu 80 wameuawa katika maandamano ya miezi mitatu ya kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro.