Polisi Ufaransa yamkamata mtu aliyejaribu kuvamia msikiti

Polisi wanasema vizuizi vilivyokuwepo nje ya msikiti vilimfanya mshambuliaji huyo kushindwa kutimiza azma yake
Image caption Polisi wanasema vizuizi vilivyokuwepo nje ya msikiti vilimfanya mshambuliaji huyo kushindwa kutimiza azma yake

Polisi nchini Ufaransa imemkamata mtu mmoja katika jiji la Paris baada ya kujaribu kuendesha gari kwa kasi mbele ya umati wa watu nje ya msikiti mmoja.

Shambulizi hilo lilitokea katika kitongoji cha Créteil na hakuna aliyejeruhiwa.

Mtu huyo hakuweza kutimiza azama yake baada ya kushindwa kuvipita vizuizi vilivyokuwepo mbele ya msikiti huo.

Image caption Polisi akiwalinda wanawake wa Kiislam waliokuwa wakitoka msikitini hapo

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema mshambuliaji huyo ana asili ya Armenia.

Lengo la shambulizi hilo bado halijajulikana.