Wabunge Ujerumani waidhinisha ndoa ya jinsia moja

Nje ya Bunge, watetezi wa ndoa za jinsia moja walisherehekea kupitishwa kwa mswada huo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nje ya Bunge, watetezi wa ndoa za jinsia moja walisherehekea kupitishwa kwa mswada huo

Wabunge nchini Ujerumani wameidhinishwa, kwa wingi wa kura, sheria ya kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Wamefanya hivyos iku chache baada ya Kansela Angela Merkel kuondoa upinzani wake dhidi ya mpango huo.

Chini ya mabadiliko hayo sasa, wapenzi wanaotaka kuoana ambao awali walikubaliwa tu kuwa na ushirika, hadhi ya ndoa kamili na wana haki ya kuasili watoto.

Wapinzani wa Bi Merkel kisiasa walikuwa wanaunga mkono sana hatua hiyo.

Lakini kansela huyo, ambaye alionekana kuunga mkono kufanyika kwa kura hiyo Jumatatu, alipiga kura ya kupinga.

Mswada huo uliungwa mkono na wabunge 393, 226 wakaupinga na wanne wakasusia.

Sheria nchini Ujerumani sasa itasoma: "Ndoa inafanikishwa na watu wawili wa jinsia tofauti au jinsia moja," shirika la habari la AFP limeripoti.

Baada ya kura hiyo ya Ijumaa, Bi Merkel amesema kwamba kwake ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke.

Lakini amesema anatumai kwamba kupitishwa kwa mswada huo kutafanikisha "utangamano zaidi wa kijamii na amani".

Wakati wa kampeni 2013, Bi Merkel alisema kwamba anapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja, kwa msingi wa "maslahi ya watoto", alkini akakiri kwamba amekuwa na wakati mgumu kuhusu suala hilo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Merkel amebadili msimamo wake kuhusu kuasiliwa kwa watoto na wapenzi wa jinsia moja, lakini bado anapinga ndoa za aina hiyo

Lakini akihojiwa na jarida moja la wanawake la Brigitte 26 Juni, alishangaza vyombo vya habari, akijibu swali la msomaji kuhusu suala hilo, aliposema kwamba amegundua vyama vingine vinaunga mkono ndoa za jinsia moja na kwamba angeruhusu kura ipigwe karibuni.

Mada zinazohusiana