Watu 2 wauawa katika maandamano Venezuela

Maandamano Venezuela Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano Venezuela

Wanaume wawili wameuwawa katika mji wa Barquisimeto huko Venezuela katika maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali kote nchini.

Zaidi ya watu 80 wameuwawa tangu kuanza maandamno dhidi ya rais Nicolas Maduro, wakati taifa hilo linakumbwa na matatizo makubwa ya kiuchumi na kisiasa.

Vyombo vya habari katika mji wa Barquisimeto vinaripoti kwamba magenge ya vijana yanayounga mkono serikali yamekuwa yakiwatishia watu.

Mjini Caracas, watu wengi walitiwa mbaroni wakijaribu kuelekea kwenye makao ya mahakama ya uchaguzi.