Trump apiga picha na wasichana wa Chibok

Rais Trump akipiga picha na wasichana wa Chibok siku kadhaa baada ya wasichana hao kufuzukatika masomo yao Haki miliki ya picha Ikulu White House
Image caption Rais Trump akipiga picha na wasichana wa Chibok siku kadhaa baada ya wasichana hao kufuzukatika masomo yao

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kupunguza ufadhili wiki aliyokutana na wasichana wawili waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram Kutoka Nigeria.

Habari hiyo imeongezea kwamba Ikulu ya Whitehouse bado haijatoa habari zozote kuhusu mkutano wa Trump na Joy Bishara na Lydia Pogu.

Inasema kuwa kitu kilichosemwa na Ikulu kuhusu ziara hiyo ni wakati walipochapisha picha hii katika mtandao wa facebook ya Ikulu ya Whitehouse ikisema kuwa ilikuwa picha ya siku.

Gazeti la People lilichapisha ujumbe wa Bi Bishara na Pogu uliosema kuwa ni miongoni mwa wasichana wachache waliofanikiwa kutoroka usiku wa kutekwa kwao na walisafirishwa hadi Marekani mnamo mwezi Agosti 2014 ili kusoma nchini humo.

Mwezi huu wasichana hao walipata vyeti vyao vya kufuzu na wanatarajiwa kujiunga na chuo kikuu cha Southeastern University mjini Florida.

Baada ya kukuzwa katika hali ya umasikini katika eneo la Chibok bila maji na kompyuta wote sasa wanasema kwamba maisha yao yamebadilika na ni kama ndoto.