Marekani yarudisha mihuri ilioibwa Korea Kusini

Mihuri ya kifalme ilioibwa Korea Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mihuri ya kifalme ilioibwa Korea Kusini

Marekani imerudisha mihuri 2 ya kifalme kwa Korea Kusini ilioibwa kutoka taifa hilo yapata miaka 60 iliopita.

Mihuri hiyo ya ufalme wa Chosun ya karne ya 16 na 17 inaminiwa kuwa na thamani ya dola milioni moja nukta tano kwa jumla.

Mihuri hio ya kifalme iliotengezwa kama kobe ilikabidhiwa rais Moon Jae-in wakati wa ziara yake mjini Washington siku ya Ijumaa.

Marekani imerudisha takriban vitu 8000 kwa zaidi ya mataifa 30 tangu 2007.

Muhuri wa zamani zaidi kati ya mihuri hiyo miwili ilioibwa ni ule wa shaba uliokabidhiwa malkia Munjeong mke wa tatu wa mfalme wa Chosun mwaka 1547.

Mfalme huyo alikuwa wa 11 na unaaminiiwa kuibwa wakati wa vita vya Korea.

Muhuri mwengine ni ule wa Jade uliotengezewa mfalme Hyeonjong mwaka 1651 na unaaminiwa kuibwa wakati Japan ilipoingia Korea kati ya 1910 na 1945.

Uchunguzi ulianza baada ya muhuri wa malkia Munjeong kupatikana katika makavazi ya mjini Los Angeles 2013.

Muhuri wa mfalme Hyeonjong ulipatikana katika makavazi ya kibinafsi.

Mihuri yote itawasili nchini Korea Kusini siku ya Jumapili na rais Moon.

Itawekwa katika maonyesho ya umma mwezi Agosti.