Rais wa Ufaransa awasili Mali

Rais wa Ufaransa awasili Mali Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Ufaransa awasili Mali

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo amewasili Mali ambako anatarajiwa kuungana na viongozi wa Afrika magharibi katika mkutano unaonuiwa kujadili maswala ya kiusalama huko nchini mali.

Miongoni mwa watakaohudhiria kikao hicho ni Viongozi, wa Mauratania,Niger ,Burkina Faso na Chad watakaokaribishwa na mwenyeji wao rais wa Mali.

Wana matumaini ya kupata msaada zaidi wa mataifa ya magharibi, kuiimarisha kikosi chao cha kikanda cha wanajeshi wapatao elfu 5000 kupambana na wapiganaji wanaotishia utawala wa maeneo hayo.

Ufaransa tayari ina wanajeshi walioko Mali tangu walipoingia nchini humo miaka minne iliyopita kwa minajili ya kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Al Qaeda .

Hata hivyo licha ya uwepo wao na vile vile kikosi cha walinda amani 10,000 kutoka Umoja wa Mataifa, sehemu kubwa ya Mali ingali inakabiliwa na changamoto za kiusalama.