Iran na kampuni ya Total kusaini mkataba wa gesi

Total Oil truck Haki miliki ya picha Getty Images

Iran inasema wanatarajia kuweka saini mkataba baina yao na kampuni kubwa ya uchimbaji mafuta na gesi Total ya ufaransa wa karibu dola bilioni tano..

Kwa mujibu wa mtakaba huo wenye thamani ya dolla billioi 5 , kampuni ya Total itaendeleza uchimbaji na uhifadhi wa gesi katika maeneo ya kusini mwa bahari ya Iran, liitwalo Pars gas ikiwa ni mojawapo ya mikataba mikubwa zaidi ya kibiashara kuwahi kufanywa na Iran tangu iondolewe vikwazo vya kiuchumi.

Mafisa wa wizara ya mafuta walisema kuwa mkataba huo ni wa kujengwa kiwanda cha gesi ambapo Total itapa asilimia 50.1.

Maafisa katika wizara husika wanasema makubaliano hayo yatawekwa saini kesho huko mjini Tehran.

Total ilikuwa mmoja wa wawekezaji wakubwa zaidi nchini Iran kabla ya vikwazo vya kimataifa vya mwaka 2006 kufuatia madai kuwa ilikuwa ikiunda zana za nyuklia.

Mwezi uliopita mkuu wa Total alisema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ni mipango ya kuwekeza dola bilioni moja nchini Iran ambaye ni mzalishaji mkubwa wa mafuta katika nchi za Opec.

Mada zinazohusiana