Watu 14 wauawa Iraq

Washambuliaji nchini Iraq Haki miliki ya picha AFP
Image caption Washambuliaji nchini Iraq

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amewaua watu 14 katika kambi moja nchini Iraq magharibi mwa jimbo la Anbar.

Jimbo hilo kuna wakati lilikuwa chini ya kundi la wapiganaji wa Islamic la majeshi ya Iraq yakafanikiwa kuukomboa mji huo.

Hata hivyo baadhi ya maeneo ndani ya jimbo hilo bado ni ngome ya wapiganaji wa IS.

Kutoka maeneo hayo, wapiganaji hao wana uwezo wa kufanya mashambulizi ndani ya jimbo hilo na hata Baghdad.