Mzozo wa Qatar na jirani zake

Mji mkuu wa Qatar, Doha Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mji mkuu wa Qatar, Doha

Qatar imesema majibu rasmi ya madai za nchi za Kiarabu yanatarajiwa kutolewa leo Jumatatu kwa mtawala wa Kuwait ambaye ni msuluhishi wa mgogoro huo mbaya kuwahi kutokea miongoni mwa nchi hizo.

Barua kutoka kwa mtawala wa Qatar itapelekwa kwa Waziri wa mambo ya nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani. Mwisho wa siku kumi ambazo Qatar ilipewa kwa ajili ya majibu ya kutoa majibu zimemalizika jana jumapili, hata hivyo ripoti zinasema muda zaidi wa saa arobaini na nane umeongezwa.

Uamuzi wa muungano wa nchi za Kiarabu ni kuitaka Doha kufunga kituo cha matangazo cha Al Jazeera, kufunga kituo cha kijeshi cha Uturuki pamoja na kuvunja uhusiano wake na Iran.

Mwezi uliopita nchi za Saudi Arabia, Bahrain, Falme za Kiarabu na Misri ziliiwekea vikwazo vya kiuchumi na kidplomasia Qatar kwa madai kuwa imekuwa ikisaidia makundi ya kigaidi madai ambayo Qatar yenyewe inayakanusha.

Hata hivyo muungano wa nchi hizo za Kiarabu wanasema kuwa wanatarajia kukutana siku ya jumatano kwa majadiliano juu hatua inayofuata dhidi ya Qatar.