Mapambano dhidi ya Ugaidi yaendelea Raqqa

vita vyajeruhi wengi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption vita vyajeruhi wengi

Ripoti kutoka Syria zimesema kikosi cha majeshi ya muungano kinachoongozwa na Marekani kimepiga hatua katika mapambano yake dhidi ya kundi la IS huko Raqqa.

Taarifa ni kuwa kundi la wapiganaji wa Syrian Democratic Forces wanaoungwa mkono na Marekani tayari wamefanikiwa kuingia katika eneo la soko la Al-Hal ambako wamemudu kukabiliana na mashambulio ya wana mgambo wa IS.

Shirika la kutetea haki za kibinadamu Syrian Observatory for Human Rights hata hivyo linasema mashambulio ya angani ya majeshi hayo ya muungano yamesababisha vifo vingine 11 hivyo kuongeza idadi ya waliofariki hadi 200 tangu vikosi hivyo kuingia katika eneo hilo.