Qatar yapewa saa 48 zaidi kutekeleza masharti ya nchi za kiarabu

Qatar yapewa saa 48 zaidi kutekeleza masharti Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Qatar yapewa saa 48 zaidi kutekeleza masharti

Saudi Arabia na nchi tatu za kiarabu zimeongeza muda kwa nchi ya Qatar, kutimiza masharti iliyopewa la sivyo iwekewe vikwazo zaidi baada ya saa 48.

Tarehe ya mwisho ya kuitaka Qatar kukubali masharti 13, ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera ilimalizika siku ya Jumapili.

Taifa hilo la ghuba linasema kuwa litajibu kupitia barua ambayo itawasilishwa kwa Kuwait leo Jumatatu.

Qatar inakana madai kutoka kwa majirani zake kuwa inafadhili itikadi kali.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini humo, atasafiri kuenda Kuwait leo, kuwasilisha barua hiyo iliyotumwa kutoka kwa emir wa Qatar kuenda kwa emir wa kuwait ambaye ndiye mpatanishi mkuu wa mzozo huo.

Image caption Qatar yapewa saa 48 zaidi kutekeleza masharti

Siku ya Jumamosi waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani, alisema kuwa taifa hilo lilikataa masharti hayo lakini liko tayari kwa mazungumzo.

Qatar imekuwa chini na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa wiki kadha sasa, kuetoka Saudi Arabia, Misri, milki ya nchi za kiarabu na Bahrain.

Kati ya masharti Qatar imetakiwa kuyatimiza ni pamoja na:

  • Kukata uhiasiano wote na kundi la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku katika nchi nyingi za kiarabu.
  • Kuacha kuwapa uraia watu kutoka nchi hizo na kuwatimua wale ambao tayari wakao nchini humo.
  • Kuwasalimisha watu wote wanaotafutwa na nchi hizo kwa sababu za kigaidi.
  • Kuacha kufadhili makundi yenye itikadi kali ambayo yameorodheshwa kuwa ya kigaidi na Marekani.
  • Kutoa taarifa za kina kuhusu watu wa upinzani ambao wamepata ufadhili kutoka Qatar hasa nchini Saudi Arabia na mataifa mengine.
  • Kuegemea katika misingi ya kisiasa na kiuchumi na baraza la nchi za Ghuba GCG.
  • Kuacha kufadhili mashirika ya habari yakiwemo Al Jazeera, Arabi21 na Middle East Eye.
  • Kulipa kiwango kisichojulikana cha pesa kama fidia.

Afisa mmoja kutoka moja ya mataifa hayo manne aliliambia shirika la Reutere kuwa Qatar pia ilikuwa imetakiwa kukata uhusiano na makundi ya Islamic State, al-Qaeda na kundi la Hezbollah nchini Lebanon.

Mada zinazohusiana