Mwanamke anusurika mashambulio matano ya tindi kali, India

In this photograph taken on 10 October 2014 burn marks are seen on the hand of Indian acid attack survivor Reshma as she rests in her home at a slum in the eastern suburbs of Mumbai. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamke anusurika mashambulizi matano ya tindi kali nchini India

Mwanamke mmoja kwenye jimbo la Uttar Pradesh nchini India ambaye aliponea kisa cha kubakwa na kundi la wanaume na visa vinne tofauti vya mashambulizi kwa tindi kali, ameshambuliwa tena na mtu ambaye alimtupia tindi kali .

Alishambuliwa nje ya makazi ya wanawake huko Lucknow alipokuwa akichota maji.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 35 amekuwa chini ya ulinzi wa polisi kufuatia mashambulizi ambayo yanatokana na mzozo wa umiliki wa mali.

Sasa ghadhabu inazidi kuelekezwa kwa mamlaka kwa kutomlinda mwanamke huyo.

Alidaiwa kubakaw na kundi la wanaume na kushambuliwa kwa tindi kali na wanaume wawili mwaka 2008 kutokana na mzozo wa umiliki wa mali.

Huwezi kusikiliza tena
Mwanamke aponea mashambulizi 5 ya tindi kali India

Wanaume hao wawili tena wanalaumiwa kwa kumshambulia kwa atindi kali mara mbili zaidi mwaka 2012 na 2013 kumlazimisha kuachana na kesi dhidi yao.

Mwezi Machi alishambuliwa tena alipokuwa akisafiri kwa treni na bintiye, na wakati huu alilazimiswa kunywa tindi kali hiyo.

Wanaume wawili walikabiliwa na mashtaka kwa visa hivyo lakini wakaondolewa mashtaka mwezi Aprili.

Kulingana na serikali kuna mamia ya visa vinavyohusu mashambulizi ya tindikali nchini India.

Image caption Mwanamke anusurika mashambulizi 5 ya tindi kali India

Mada zinazohusiana