Willy M Tuva: Siri ya ufanisi kimuziki Afrika Mashariki
Huwezi kusikiliza tena

Mawaidha ya 'Mzazi' Willy Tuva kwa wasanii wa kizazi kipya

Muziki wa kizazi kipya Afrika mashariki unaendelea kukua kwa viwango. wasanii kama vile sauti sol wa kenya, Diamond wa Tanzania na Chameleon wa Uganda wamekuwa mabalozi wa muziki huo duniani kote.

Lakini je, siri yao ni ipi wakilinganishwa na wasanii wengine hususan kutoka mataifa mengine ya kanda hii kama vile Rwanda, Burundi na Sudan Kusini?.

Anthony Irungu amezungumza na mtangazaji wa redio na runinga Willy M Tuva kutoka Kenya.