Watu 18 wafariki baada ya basi kuteketea Ujerumani

Hof Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mabaki ya basi lililokuwa limewabeba wazee

Watu 18 wamefariki baada ya basi walimokuwa wakisafiria kugongana na lori na kushika mojo katika barabara moja kusini mwa Ujerumani.

Watu wengine 30 waliokuwa kwenye basi hilo walijeruhiwa na wawili kati yao wamo katika hali mahututi.

Basi hilo lilikuwa limewabeba wazee wakati wa kutokea kwa ajali hiyo karibu na Stammbach kaskazini mwa Bavaria.

Waziri wa mambo ya ndani wa Bavaria Joachim Herrmann amesema maafisa wa uokoaji walicheleweshwa na wenye magari wengine ambao walikuwa wanaendesha magari yao kwa mwendo wa pole na pia ukali wa moto huo.

Chanzo cha moto huo hakijabainika.

Magari yalikuwa yanasonga kwa mwendo wa pole wakati wa kutokea kwa ajali hiyo.

Lori lililohusika kwenye ajali hiyo pia liliteketea.

Mtandao mmoja wa habari Ujerumani Frankenpost umeripoti kuwa gari hilo lilikuwa limebeba mito na godoro.

Dereva wa lori hakuumia na ameambia polisi kwamba alikuwa ameenda sehemu ya nyuma ya gari hilo kulikagua lilipolipuka na kushika moto.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabaki ya basi na lori hilo
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wataalamu wakichunguza mabaki ya basi na miili ya watu iliyoteketea
Haki miliki ya picha Reuters
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Helikopta tano za maafisa wa huduma za dharura zilifika eneo la ajali

Bus crash scene on A9 near Hof (3 July)

Mada zinazohusiana