Polisi wachunguza mauaji ya wenye vipara

mauaji ya watu wenye vipara Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption mauaji ya watu wenye vipara

Polisi katika jimbo la Zambezia nchini Msumbiji wamewakamata watu wa nne kwa kuhusika na mauaji ya watu wenye vipara.

Wamesema wanaendelea pia na uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo huku wakifuatilia zaidi kujua nani anachochea mauaji hayo.

Waganga wa kienyeji wamekuwa wakidaiawa kusambaza habari zisizo na ukweli kwamba vichwa vya watu wenye vipara vimekuwa na dhahabu.

Polisi nchini Msumbiji pia wamekuwa wakichunguza mauaji ya Albino ambao wanakatwa viongo vyao vya mwili, na kutumika katika masuala ya imani za kishirikina.

Aidha wamesema washukiwa hao wa auaji wanatoka katika nchi jirani.