Gari latumbukia kwenye bwawa la kuogelea

Gari latumbukia katika Bwawa la kuogelea Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari latumbukia katika Bwawa la kuogelea

Mwanamke mmoja nchini Marekani amejikuta akilitumbukiza gari lake katika bwawa la maji ya kuogelea baada ya kuripotiwa kukanyaga mafuta badala ya breki za gari.

Ripoti zinasema gari hilo liligonga nyingine, na kujilkuta likiongeza kasi hadi katika eneo hilo la kitalii katika jimbo la Colorado, na kuvuka uzio, hatimaye kuangukia katika bwawa hilo la kuogelea.

Hakuna mtu aliyekuwepo eneo hilo wakati gari hilo likitumbukia, huku dereva wa gari hilo ambaye aliokolewa, akifikishwa hospital akiwa na majeraha madogo.

Hata hivyo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka kwa kuendesha gari vibaya na kusababisha hatari.

Shuhuda wa ajali hiyo Jessica Puzio ambaye alikuwa mgeni katika eneo hilo la kitalii ameiambia BBC kuwa wakati akienda na rafiki yake katika eneo hilo la kuogelea, walishikwa na butwaa baada ya kuona gari likiwa limezama kwenye maji.

Anasema cha ajabu gari hilo pia lilikuwa likionesha halikuwa limepata madhara, licha ya matairi kuonesha kuishiwa upepo.

Haki miliki ya picha copyrightINSTAGRAM/FREDD1E
Image caption Maji ya Bwawa la Kuogelea yatolewa

Hata hivyo maji katika bwawa hilo la kuogelewa yalitolewa kuwezesha gari hilo kutolewa