Hatma ya wanariadha wa kike wenye homoni nyingi za kiume kujulikana

Mwanariadha wa mita 800 kutoka Afrika Kusini Caster Semenya
Image caption Mwanariadha wa mita 800 kutoka Afrika Kusini Caster Semenya

Utafiti mpya unasema kuwa wanawake wanaozaliwa na viwango vya juu vya homini za kiume {Testosterone} wana uwezo mkubwa wa utendaji ikilinganishwa na wenzao katika mashindano.

Ripoti hiyo iliochapishwa katika jarida la matibabu katika michezo inatokana na sampuli 100 za damu zilizochukuliwa kutoka kwa wanariadha katika kipindi cha miaka miwili.

Imechapishwa wiki chache kabla ya mahakama ya usuluhishi kuhusu maswala ya michezo kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu uamuzi wa shirikisho la wanariadha duniani I.A.A.F kuwapiga marufuku wanariadha wa kike walio na homoni nyingi za testosterone.

Marufuku hiyo ilioanzishwa 2011,ilisitishwa na mahakama hiyo miaka miwili iliopita.

Watafiti wake wanasema kuwa ushirikiano kati ya viwango vya juu vya homini za testosterone na utendaji bora haufai kuchukuliwa kama thibitisho.