Ndege ya AirAsia X yalazimika kurudi ilikotoka kufuatia wasiwasi wa abiria

Ndege ya AirAsia X yalazimika kurudi ilikotoka kufuatia wasiwasi wa abiria Haki miliki ya picha ABC
Image caption Ndege ya AirAsia X yalazimika kurudi ilikotoka kufuatia wasiwasi wa abiria

Ndege ya kampuni ya Air Asia X iliokuwa ikielekea Kuala Lumpur ililazimika kurudi nchini Australia baada ya kindege kuwatia wasiwasi abiria.

Ndege hiyo iliokuwa na abiria 359, ilipata matatizo baada ya kupaa siku ya Jumatatu.

Abiria waliripoti kusikia kelele kubwa na kuona miale ya moto ikitoka katika mashine ya ndege hiyo kabla ya kutua salama katika mji wa Brisbane nchini Australia saa moja baadaye.

Ndege iliyokuwa ikitingishika yalazimika kutua Australia

Mabaki ya ndege wawili yalipatikana katika barabara ya ndege hiyo, kulingana na kampuni hiyo.

Abiria mmoja Tim Joga alisema alihisi milio minne ya kelele kati ya mitano na mwangaza mwingi, aliambia jarida la kila asubuhi la Morning Herald.

Abiria mwengine Eric Lim alisema kuwa kisa hicho kilitokea muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa.

Image caption Ramani ya Australia na Malaysia

''Kulikuwa na miale ya moto na sauti za boom boom boom na watu wakaanza kulia na kusema 'Mungu wangu' 'mungu wangu'',aliandika katika mtandao wake wa facebook.

Mkurugenzi wa kampuni ya AirAsia X Benyamin Ismail alisema kuwa rubani na wafanyikazi wa ndege walichukua hatua ya kuwahakikishia abiria wakati wa kisa hicho.

''AirAsia X sasa itapanga ndege maalum ya kuwasafirisha wageni wote katika ndege D7 207 inayoelekea Kuala Kumpur haraka iwezekanavyo'',alisema katika taarifa.

Wiki iliopita ndege ya AirAsia X ililazimika kurudi Perth baada ya tatizo la mashine kuifanya itetemeka ''kama mashine ya kuosha nguo''.

Haki miliki ya picha ABC
Image caption Ndege aina ya AirAsia X

Mapema mwizi huu ndege ya China Eastern Airline ilitua kwa ghafla mjini Sidney baada ya shimo kubwa kuonekana katika mashine yake.

Mnamo mwezi Disemba 2014 ndege aina ya AirAsia ilianguka katika bahari ya Java na kuwaua abiria 162 baada ya mfumo wa rada wa ndege hiyo kutofanya kazi ilipokuwa angani.