Bondia aliyemshinda Manny Pacquiao asema hakupendelewa

Bondia Horn wa Australia akimzaba makonde makali Manny Pacquiao Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bondia Horn wa Australia akimzaba makonde makali Manny Pacquiao

Mwalimu wa zamani aliyempiga Manny Pacquiao ili kushinda taji la uzani wa welterweight ukanda wa WBO amepuuzilia mbali madai kwamba hakufaa kushinda taji hilo.

Jeff Horn alimshinda Pacquiao, bingwa wa dunia mara nane, kufuatia wingi wa pointi katika mji wa Brisbane, Australia.

Mkufunzi wa Pacquiao na watu maarufu akiwemo Lennox Lewis na Kobe Bryant walikosoa matokeo hayo.

Lakini bondia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 29 alisema kuwa alihitaji kushinda.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bondia Jeff Horn aliyemshinda Manny Pacquiao kwa wingi wa pointi

Kutakuwa na maneno kwamba nilikuwa na bahati ama chchote kile, aliwaambia maripota siku ya Jumatatu.

Kutakuwa na wale watakaosema kwamba sikuhitaji kushinda, lakini ninahisi kwamba nilishinda pigano hilo.

Wananchi wengi wa Queensland wanajua kwamba nilishinda pigano hilo pamoja na watu wote duniani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manny Pacquiano baada ya pigano hilo

Kocha wa Pacquiao nchini Australia Justine Fortune alitaja uamuzi wa refa na majaji kama usio wa haki kufuatia pigano hilo.