Wanawake watakiwa kuvalia nadhifu Uganda

Sheria mpya za mavazi kwa wafanyakazi wa umma Uganda
Image caption Sheria mpya za mavazi kwa wafanyakazi wa umma Uganda

Wizara ya utumishi wa umma nchini Uganda imewafahamisha wafanyakazi wa serikali kuvalia nadhifu na kuwaonya wanawake dhidi ya kuonyesha vifua vyao.

Kupitia ilani rasmi, wizara hiyo imesemaa wanawake hawaruhusiwi kuvalia nguo au sketi ambazo zinafika juu ya magoti yao, pamoja na nguo zilizoshonwa kwa kitambaa cha kuonesha mwili ndani.

Wanawake wanaruhusiwa kuvalia suti za long'i, lakini wale walio wafanyakazi wa serikali hawaruhusiwi kuvalia mavazi ya kuwabana.

Ilani hiyo inasema kuwa mavazi ya urembo yanastahili kuwa nadhifu na wanawake hawaruhusiwi kupaka nywele zao rangi inayong'aa au kuwa na nywele ya kuongezwa.

Wanaume nao watakiwa kuvalia nadhifu, shati za mikono mirefu, koti na tai, wasivae suruali za kubana, wawe na nywele fupi na safi na wasivae mavazi ya rangi zinazong'aa.

Hata hivyo masharti hayo hayajaonekana kuanza kufuatwa hadi sasa.

Mada zinazohusiana