Wachimba mgodi 17 wakwama ardhini Ghana

Wachimba mgodi 17 wakwama ardhini Ghana Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachimba mgodi 17 wakwama ardhini Ghana

Watoa huduma za dharura nchini Ghana wanajaribu kuwaokoa wachimba mgodi 17 waliokwama ndani ya mgodi mmoja tangu siku ya Jumapili.

Mgodi huo ulio eneo la Prestea-Nsuta magharibi mwa nchi, uliporomoka na kuwafunika wachimba migodi hao umbali ya mita 25 ardhini.

Watano kati yao walifanikiwa kujiokoa kutoka kwa mgodi huo.

Uchimbaji madini unaofanywa kinyume na sheria na unaodaiwa kuendeshwa na raia wa China, ni suala linalozua wasi wasi kwa mamlaka za Ghana kutokana na sababu za kiusalama na athari zake kwa mazingira.

Watu kadha wamekamatwa na vyombo kushikwa. Serikali sasa imebuni jopo kuchunguza tatizo hilo huku idadi ya ajali zikiongezeka.