Waziri mkuu wa India Narendra Modi afanya ziara nchini Israel

Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu (2nd R) welcomes Indian Prime Minister Narendra Modi (2nd L) during an official welcoming ceremony upon his arrival in Israel at Ben Gurion Airport, near Tel Aviv, Israel 4 July 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa India afanya ziara nchini Israel

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amewasili nchini Israel , na kuwa waziri wa kwanza kwa India kufanya ziara nchini Israeli.

Bwana Modi ambaye juzi alisema kuwa India na Israel zina uhusiano wa miaka mingi anatarajia kusaini makubaliano ya kijeshi na usalam wa mitandao.

Bwana Modi hatasafiri kuenda Ramallah au kukutana na viongozi wa Palestina kama wageni wengine hufanya.

Ziara hiyo inaonekana kuwa mabadiliko makubwa kwa msimamo wa India kwa Israel.

Modi atakuwa nchini Israel kwa siku tatu.

Kwa miaka mingi Israel na India wamekuwa wakishirikiana katika masuala ya kupambana na ugaidi na ulinzi na India imekewa mteja wa kununua silaha kutoka taifa hilo la kiyahudi.

Ikijitahidi kuboresha jeshi lake kukabiliana na China na Pakistan, India sasa ndiye mnunuzi mkuwa wa silaha za Israel zenye gharama inayokisiwa kuwa ya dola bilioni moja.