David Beckham ajitetea kwa kumpiga busu mwanawe

David Becham akimpiga busu mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka mitano mdomoni
Image caption David Becham akimpiga busu mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka mitano mdomoni

David Beckham akimpiga busu mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka mitano mdomoni

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United alikosolewa kwa kuchapisha picha akimpiga busu la mdomoni mwanawe wa kike Harper katika mtandao wa Instagram.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja kupitia mtandao wa facebook, Beckham alisema kuwa ''tunataka kuwaonyesha wana wetu mapenzi''.

Mkewe David Beckham, Victoria pia alikosolewa kwa kuchapisha picha akimpiga busu mdomoni mtoto huyo wa kike mwaka uliopita

Haki miliki ya picha Instagram
Image caption Mkewe David Becham, Victoria pia alikosolewa kwa kuchapisha picha akimpiga busu mdomoni mtoto huyo wa kike mwaka uliopita

''Nilikosolewa kwa kumpiga busu mwanangu mwaka uliopita'',alisema.

''Pengine siwezi kumfanyia hivyo Brooklyn mwenye umri wa miaka 18 kwa kuwa ataona kama swala la kushangaza.Lakini nina mapenzi tele na wanangu''.

''Hivyo ndivyo nilivyolewa na Victoria na hivyo ndivyo tulivyo na watoto wetu''.

''Tunataka kuwaonyesha watoto wetu mapenzi na kuwalinda, kuwaangalia na kuwasaidia na unajua tuna mapenzi tele nao''.

Nyota wa filamu kutoka nchini Marekani Hilary Duff pia alipokea matusi mwaka uliopita baada ya kupigwa picha akimpiga busu mwanawe wa kiume katika eneo la Disneyland California.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Nyota wa filamu kutoka nchini Marekani Hilary Duff pia alipokea matusi mwaka uliopita baada ya kupigwa picha akimpiga busu mwanawe wa kiume katika eneo la Disneyland California.

Kulikuwa na ujumbe uliomkosoa chini ya picha hiyo, lakini akijibu katika mtandao wa Instagram ,Hillary alitetea hatua yake ya kumpiga busu mwanawe.

Haki miliki ya picha Instagram
Image caption Hilary Duff aliwajibu wakosoaji wake

Beckham pia alisema kwamba alifurahia kazi ya kupiga picha ya Brooklyn baada ya kazi yake kukosolewa.