Wachoraji vibonzo wamshambulia Trump Iran

Hadi Asadi kutoka Iran, akimuonyesha rais huyo wa Marekani akiwa amevalia koti la noti za dola za Marekani mbali na kuvaa nywele za manjano zinazochomeka.
Maelezo ya picha,

Hadi Asadi kutoka Iran, akimuonyesha rais huyo wa Marekani akiwa amevalia koti la noti za dola za Marekani mbali na kuvaa nywele za manjano zinazochomeka.

Trump akejeliwa Iran katika mashindano ya uchoraji vibonzo

Mamia ya wachoraji duniani wameshiriki katika mashindano nchini Iran ya kumshambulia Donald Trump.

Mchoro ulioshinda, ulichorwa na Hadi Asadi kutoka Iran, ukimuonyesha rais huyo wa Marekani akiwa amevalia koti la noti za dola za Marekani mbali na kuvaa nywele za manjano zinazochomeka.

Waratibu wa maonyesho hayo jijini Tehran wamewahi kuaandaa mashindano kama hayo yakiwa na mandhari ya IS pamoja na mauaji ya halaiki Ujerumani.

Nembo ya mwaka huu ililingana na alama ya Nazi, ikiwa na T badala ya swastika.

Maelezo ya picha,

Nembo ya mwaka huu ililingana na alama ya Nazi, ikiwa na T badala ya swastika.

Ilihamasisha kulinganishwa kwa rais wa Marekani na Unazi.

"Wengi wanaamini misemo yake inafanana na ya Hitler. Amekuwa na mtazamo mbaya kuhusu mashirika ya habari na wakimbizi, Mratibu Masoud Shojai Tabatabaei aliiambia shirika la habari la Associated Press.

Maelezo ya picha,

Nembo hiyo iIlihamasisha kulinganishwa kwa rais wa Marekani na Adolf Hitler

Mandhari ya mwaka jana katika mashindano hayo ya uchoraji vibonzo yalivutia hisia kali kutoka kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Lakini waandalizi walisema wanafurahia kuonyesha misimamo yao kuhusu uhuru wa kujieleza kuliko kutilia shaka mauaji ya halaiki yaliyofanyika Ujerumani.

Mtazamo wa wengine katika mashindano ya mwaka huu ulitolewa kwa ahadi za Trump za kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico, vile vile unyanyasaji wa wanawake na kupiga vita vyombo vya habari.

Maelezo ya picha,

Mtazamo wa wengine katika mashindano ya mwaka huu ulitolewa kwa ahadi za Trump za kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico

Maelezo ya picha,

Rais huyo wa Marekani ameonyeshwa akimlazimisha Melania Trump kutabasamu kwa kitumia mikufu ya dhahabu

Maelezo ya picha,

Kibonzo hiki kinamuonyesha rais Trump akiwa mtoto

Baadhi ya walioshiriki walikuwa wachoraji vibonzo kutoka Marekani na Uingereza.

Clayton Jones, mchoraji kutoka Marekani alionyesha picha za Trump na Hitler wakiwa kwa kurasa ya mbele ya jarida la Times, Trump akimwambia

"ni heshima kubwa" naye Hitler anamjibu "ndio".

Maelezo ya picha,

Kazi za walioshiriki katika uchoraji wa vibonzo hivyo vya rais Trump