Volvo kuanza kuunda magari yanayotumia umeme ufikapo mwaka 2019

Volvo car, Shanghai Auto Show Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gari la Volvo kwenyr maonyesho China

kampuni ya kuunda magari ya Volvo imesema kuwa magari yake mapya yatakuwa yanatumia umeme kuanzia mwaka 2019.

Kampuni hiyo ya kichina imekuwa kampuni ya kwanza ya zamani iliyoanza kusitisha uundaji wa magari ya zamani yanayotumia mafuta.

Ina mipango ya kuzindua aina tano ya magari yanayotumia umeme kati ya mwaka 2019 na 2021 na mengine yanayotumia umeme na mafuta.

Lakini pia itakuwa ikiunda magari ya zamani yanayotuumia mafuta.

Volvo ina mipango ya kuuza magari milioni moja yanayotumia umeme ifikapo mwaka 2025.

"Tangazo hili liaadhimisha mwanzo wa misho wa injini za zinazotumia mafuta," amesema Hakan Samuelsson, mkurugenzi mkuu wa kitengo cha kuunda magari ya Volvo.

Hii ni baada ya kampuni ya Marekani ya Tesla kutangaza Jumapili kuwa itaanza kuuza magari yake yanayotumia umeme ya Model 3 ifikapo mishoni mwa mwezi huu.

Elon Musk, mwanzilishi wa Tesla alifanikiwa kuunda magari 20,000 ya Model 3 kila mwezi hadi Disemba iliyopita.

Mada zinazohusiana