Al-Shabab wapigana na vikosi vya ulinzi Kenya

Al-Shabab wapigana na vikosi vya ulinzi Kenya Haki miliki ya picha AFP
Image caption Al-Shabab wapigana na vikosi vya ulinzi Kenya

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab wameshambulia kituo cha polisi katika mji wa wa pwani ya kenya wa Lamu ulio karibu na mpaka wa Somalia.

Vikosi tofauti vya usalama nchini Kenya vilichukua hatua za haraka kufuatia fununu kuwa eneo hilo lingeshambuliwa.

Kulingana na mkuu wa polisi nchini Kenya, Joseph Boinett, shambulio hilianza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, ambapo washambulizi wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la alshabaab walivamia kituo cha polisi cha pandanguo, Lamu magharibi pwani ya Kenya.

Inaarifiwa kwamba maafisa wawili wa polisi wameuwawa, na wengine saba hawajulikani waliko.

Washambuliaji hao aidha waliteketeza kituo cha polisi cha pandanguo na wakaharibu mtambo wa mawasiliano katika eneo hilo usiku wa kuamkia leo.

Mapigano makali yaliyodumu saa kadha yaliyotokea na mitambo ya mawasiliano ikaharibiwa, hali iliyosababisha kuwa na ugumu wa kupata habari.

Wakaazi wengi wa eneo hilo la Pandanguo walitorokea msitu wa Boni na wengi wao hadi sasa hawajulikani waliko.

Kulishuhudiwa ufyatulianaji mkali wa risasi majira ya asubuhi wakati maafisa wa usalama wakiwemo wanajeshi walipojibu shambulizi hilo.

Alshabaab wamekiri, kupitia mitandao, kwamba ndio waliotekeleza shambulio hilo.

Inaaminika kwamba wanamgambo hao huwa wanajificha kwenye msitu mkubwa wa Boni ambao uko karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Mada zinazohusiana