JAY-Z athibitisha mamake ni mpenzi wa jinsia moja

Mwanamuziki wa mtindo wa Rap JAY-Z Haki miliki ya picha Google
Image caption Mwanamuziki wa mtindo wa Rap JAY-Z

Msanii wa muziki wa Rap JAY-Z ameonekana kuthibitisha kuwa mamake ni mpenzi wa jinsia moja

Kulingana na maneno ya wimbo wa albamu yake 4:44, msanii huyo alisema:Mama alikuwa na watoto wanne lakini ni mpenzi wa jinsia moja licha ya kujifanya kuwa muigizaji.

Haijalishi kwangu iwapo ni mume ama mke nataka kukuona ukifurahi baada ya chuki zote.

Mapema katika kipindi chake chote cha kazi ya muziki JAY-Z aliandika nyimbo zilizokuwa na maneno ya watu wa mapenzi ya jinsia moja lakini akawacha kurekodi nyimbo zenye maneno hayo

Maneno hayo ya muziki yapo katika wimbo unaoitwa Smile ambao pia unashirikisha picha ya mamake Gloria Carter akisoma shairi.

Ni nani ambaye JAY- Z hakumshukuru baada ya kupata tuzo yake ya hivi karibuni?

Image caption JAY-Z na mkewe Beyonce

Kutokana na uwepo wake katika wimbo huo ,inaonekana kwamba alijua kuhusu mpango wa mwanawe kuzungumzia kuhusu jinsia yake.

''Dunia inabadilika na wanasema ni wakati wa kuwa huru/lakini unaishi na hofu ya kuwa wewe mwenyewe'', alisema mamake.

''Kuishi katika kivuli kunaonekana kuwa eneo salama kuwa, hakuna mtu wa kukushambulia /lakini maisha ni mafupi na ni wakati wa kuwa huru''.