Uvumi kuhusu mchele wa plastiki kuuzwa nchi za Afrika

Uvumi wa mchele bandia kuuzwa nchi za Afrika Haki miliki ya picha YOUTUBE
Image caption Uvumi wa mchele bandia kuuzwa nchi za Afrika

Licha ya kuwepo ushahidi kuwa ni tatizo kubwa, uvumi kuhusu mchele wa plastiki kuuzwa barani Afrika na sehemu zingine zinazidi kukita mizizi.

Uvumi uliendelea wiki kadha zilizopita nchini Senegal, Gambia na Ghana hadi kiwango kilichosabisha halmashauri ya chakula nchini Ghana kufanya uchunguzi.

Waliwaalika watumiaji na wafanyabiashara kusalimisha sampuli za mchela walioshuku kuwa umetengenezwa kwa plastiki na baadaye wakatangaza kuwa hakukuwa na mchele wa pastiki kwenye masoko nchini Ghana.

Uvumi kwenye mitandao ya kijamii umekuwa ukisambaa tangu mwaka 2010 kuhusu mchele wa plastiki kutengenezwa na kuchanganywa na mchele halali kama njia ya kuwahadaa watumiaji.

Haki miliki ya picha YOUTUBE
Image caption Uvumi wa mchele bandia kuuzwa nchi za Afrika

Uvumi huo ulisababisha kutokea kwa sakata za mchele bandia licha ya uvumi huo kutohusu chakula kinachotengenezwa kutoka kwa plastiki.

Kisha mwaka 2011 ripoti zikaibuka kuwa mchele huo ulikuwa ukitengenezwa kutoka kwa viazi na kushikanishwa pamoja na gundi ya viwandani.

Lakini uvumi huo umekuwa ukiendelea kuwa plastiki inauzwa kama mchele, na kuchochewa na kanda za video zinazoonyesha watu wakirusha mipira ya mchele, zingine zikidaiwa kuonyesha jinsi mchele huo unatangenezwa viwandani.

Haki miliki ya picha YOUTUBE
Image caption Uvumi wa mchele bandia kuuzwa nchi za Afrika