Trump ailaumu China kwa kufanya biashara na Korea Kaskazini

This handout photo taken on 5 July 2017 and provided by South Korean Defence Ministry in Seoul shows US M270 Multiple Launch Rocket System firing an MGM-140 Army Tactical Missile from an undisclosed location on South Korea's east coast during a South Korea-US joint missile drill aimed to counter North Koreas ICBM test. Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Marekani na Korea Kusini walifyatua makombora ya masafa marefu kuenda bahari ya Japan

Rais wa Marekani ameishutumu China kufuatia hatua ya Korea Kaskazini kulifanyia majaribio kombora la masafa marefu, na kuilaumu kwa kuendelea kufanya biashara na Korea Kaskazini.

Marekani na Korea Kusini zilifanya majaribio ya makombora ya masafa marefu katika bahari ya Japan kujibu hatua hiyo ya Korea Kaskazini.

China na Urusi wamezitaka pande hizo kuacha kuonyesha ubabe wao wa kijeshi na kusema wanapinga majaribio yoyote ya kubadilisha uongozi nchini Korea Kaskazini.

Jaribio la kombora ambalo ni la hivi pudne kati ya majaribio kadha, lilienda kinyume na marufuku ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kombora la ICBM lililofyatuliwa na Korea Kaskazini

Marekani imetaka kufanyika mkutano wa dharura na baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kujadili suala hilo.

Trump alifanya mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping katika makao yake ya kifahari huko Florida mwezi Aprili.

Korea Kaskazini: Kombora letu linaweza kufika Marekani

Trump alisifu hatua alizopiga na China baada ya mkutano huo.

Takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa biashara kati ya China na Korea Kaskazini.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Trump sasa aneelekea nchini Poland na Ujerumani ambapo atakutana na Bwana Xi kwa mara ya pili.

Rais Trump sasa aneelekea nchini Poland na Ujerumani ambapo atakutana na Bwana Xi kwa mara ya pili.

China ambaye ni mshirika mkubwa wa kiuchumi wa Korea Kaskazinia na Urusi, imetaka Korea Kaskazini kuachana na progamu yake ya makombora ya masara marefu.

Bwana Xi na rais wa Urusi Vladimir Putin waliokutana mjni Moscow siku ya Jumanne walisema pande hizo zinastahili kuanza mazungumzo.