China: Nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini sio chaguo

Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Liu Jieyi Haki miliki ya picha UN web TV
Image caption Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Liu Jieyi

Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa amekiambia kikao cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba suluhu ya nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini haifai kupewa kipao mbele, akijibu hatua ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la masafa marefu.

Liu Jieyi alirejelea wito wa China na Urusi kwa mazungumzo ya Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora iwapo Marekani na Korea Kusini zitasitisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Awali balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Nikki Haley alisema kuwa vikwazo vya kimataifa vilivyowekewa Pyongyang kwa miaka kadhaa havitoshi.

Amesema kuwa vitendo vya Korea Kaskazini ni ishara za kuzuka kwa mgogoro duniani.