Watu 80 wafariki katika ajali ya barabarani CAR

Jamhuri ya Afrika ya kati CAR
Image caption Jamhuri ya Afrika ya kati CAR

Ajali ya lorry moja la mizigo huko Jamhuri ya Afrika ya kati CAR imesababisha vifo vya zaidi ya watu 80, wengi wakiwa wachuuzi waliokuwa wakielekea sokoni mjini Bambari.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema lorry hilo lilikuwa limebeba watu wengi na kujazwa mizigo kupindukia huku likiendeshwa kwa mwendo wa kasi wakati lilipopenduka.

Maafisa wa tarifiki wamelaumiwa kwa kutochukua hatua kuzuia ukiukwaji huo wa sheria za barabarani.