Manchester United yamsaka Romelu Lukaku

Romelu Lukaku anasakwa na klabu ya Manchester United Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Romelu Lukaku anasakwa na klabu ya Manchester United

Everton's Romelu Lukaku ni mchezaji ambaye huenda akasajiliwa na Mourinho huku Manchester United ikiendelea kumsaka mshambuliaji.

Mchezaji huyo ,mwenye umri ya miaka 24 alikuwa katika orodha ya washambuliaji iliowasilishwa kwa naibu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward na kocha Jose Mourinho.

Ilidhaniwa kwamba Lukaku ambaye alifunga mabao 25 msimu uliopita angejiunga tena na klabu yake ya zamani Chelsea.

Hatahivyo United sasa wanahisi kwamba inawezekana kumpata mshambuliaji huyo wa Ubelgiji.

Klabu hiyo imekuwa katika mazungumzo ya kumsajili Alvaro Morata kutoka Real Madrid lakini wameshindwa kuafikiana kufikia sasa.

Klabu ya United tayari imeanza kuwasiliana na Everton kuhusu mkataba wa aliyekuwa nahodha wa Uingereza Wayne Rooney, ambaye huenda akaondoka Old Trafford na kurudi Goodison Park.

Hatua hiyo inaweza kufanya mazungumzo kuwa rahisi ,hata iwapo kiwango cha fedha kinachozungumziwa kinaweza kuwa juu ya kiwango cha uhamisho wa pauni milioni 89 cha Paul Pogba kujiunga na United.